Monday, February 27, 2012

Na John Gagarini, Kibaha




WATU wenye ulemavu wa kutoona wilayani Kibaha mkoani Pwani

wameipongeza serikali kwa kutafsiri kwa lugha ya alama sheria mpya ya

ugonjwa wa Ukimwi ya mwaka 2008.



Mratibu wa mradi huo kwa watu wasioona wilayani humo Bw Robert Bundala

alisema kuwa kwa muda mrefu sheria nyingi zilikuwa hazijatafsiriwa kwa

lugha hiyo maarufu kama nukta nundu hali ambayo ilikuwa haiwapi nafasi

ya kujua sheria hizo.



Bw Bundala alisema kuwa kutokujua sheria hizo kulisababisha kushindwa

kujua mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na haki zao za kimsingi.



"Tunaishukuru serikali kwa kutukumbuka kwani sasa watu wasioona

wanaweza kuisoma na kujua kilichomo na kuweza kudai haki zao ambazo

wanastahili katika sheria hiyo ambayo itakuwa ikielezea juu ya namna

ya kukabiliana na ugonjwa huo na kujilinda," alisema Bw Bundala.



Alisema kuwa mbali ya kutafsiriwa kwa lugha yao ambayo imewarahishia

kuielwa pia mwanzo ilikuwa kwa lugha ya Kiingereza lakini kwa sasa

imeandaliwa kwa Kiswahili na imekuja kwa wakati muafaka.



"Watu wasioona walikuwa kwenye wakati mgumu kutokana na maumbile yao

kwani walikuwa hawajui kilichomo wala haki zao kupitia sheria hiyo,"

alisema Bw Bundala.



Mratibu huyo alisema kwa sasa wanafanya mafunzo kwa wanachama zaidi ya

300 pamoja na viongozoi wote kuanzia ngazi ya kata hadi vijiji ili

kuijua waweze kuitekaleza katika ngazi zao.



"Tumewashirikisha viongozi hao pamoja na wale wa kisiasa wakiwemo

madiwani kwani wao ndiyo wanaoandaa mipango mbalimbali kwenye jamii

ili nao waweze kunufaika," alsiema Bw Bundala.



Aliitaka jamii kubadili mwelekeo kwa kuwasaidia ili waweze kujikwamua

na mazingira magumu waliyonayo kutokana na maumbile yao na kutowaona

kama mzigo ndani ya jamii ambapo wao wanauwezo kama wale wasio na

ulemavu.



mwisho.

0 comments:

About This Blog

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP