Monday, February 27, 2012

WATU tisa wamekufa na wengine saba kujeruhiwa kwenye ajali mbili

Na John Gagarini, Kibaha




WATU tisa wamekufa na wengine saba kujeruhiwa kwenye ajali mbili

tofauti zizilzotokea juzi mkoani Pwani.



Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoani humo Bw Salehe Mbaga

alibainisha hayo jana mjini Kibaha alipokuwa akizungumza na waandishi

wa habari na kusema kuwa ajali hizo zilitokea kwenye wilaya ya Kibaha

na Rufiji.



Kamanda Mbaga alisema kuwa kwenye ajali ya kwanza amabyo ilitokea eneo

la shamba la Mpunga Mlandizi wilayani Kibaha ilisababisha vifo vya

watu saba.



Alisema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 4:00 usiku na kuyahusisha

magari mawili likiwemo basi dogo aina ya Hiace namba T 546 BGT

likiendeshwa na Bw Ramadhan Kania (52) lililokuwa likitoka Msata

kwenda Dar es Salaam liligongana na lori aina ya Scania lenye namba T

165 APQ na tela lake namba T 667 APT lililokuwa likielekea mkoani

Mwanza likiendeshwa na dereva asiyefahamika.



"Chanzo cha ajali hiyo mbaya ni dereva wa lori hilo kulipita gari

jingine kisha kukutana uso kwa uso na basi hilo dogo na kusababisha

vifo vya watu hao ambao walikufa papo hapo," alisema Kamanda Mbaga.



Aliwataja waliokufa kuwa ni Baina Goyayo, Zengeni Ramadhan, Tabia

Halfan, Sadiq Rajab, dereva wa basi dogo Bw Ramadhan Kania na wanawake

watatu ambao bado hawajatambuliwa.



Aliwataja majeruhi kuwa ni Bw Joseph Sebastian wa Chalinze, Bi Zainab

Athuman (33) wa Kwa Mfipa na mtoto Fatuma Ally mwenye umri wa mwaka

mmoja na nusu.



Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wa kasi wa lori hilo na kulipita gari

jingine bila ya tahadhari polisi wanamtafuta dereva huyo na miili na

majeruhi wako kwenye hospitali ya Tumbi.



Kwenye tukio la pili watu wawili wamekufa na wengine wanne kujeruhiwa

baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka.



Kamanda Mbaga alisema kuwa ajali hiyo ilitokea Februari 26 mwaka huu

majira ya saa 10 jioni huko Kimbunga barabara ya Kibiti - Mkongo

wilayani Rufiji.



Alisema kuwa ajali hiyo ililihusisha gari aina ya Nissan Pick Up lenye

namba za usajili T 915 Adu likiendeshwa na Bw Ben Nyaki (36) mkazi wa

Kilimanjaro likitokea Kibiti kwenda Kijiji cha Ngulakula liliacha njia

na na kugonga kingo za barabara na kusababisha vifo hivyo.



Aliwataja waliokufa kuwa ni dereva wa gari hilo Bw Nyaki na Bw Rashid

Ngukulilaga (21) mkulima wa Ruha mkazi wa Lindi Mjini.



Aliwataja majeruhi kuwa ni Bw Bashiru Namori (26) mkazi wa Ruha, Bi

Salma kambangwa (26) mkulima wa Gulakula, Bw Halfan Seleman (21) mkazi

wa Ruha na Bi Somoe Madae (27) mkulima wa Ruha.



Aliongeza kuwa watu tisa walitibiwa na kuruhusiwa kuondoka kwenye

hospitali ya Mchukwi huku miili ya marehemu ikiwa imehifadhiwa kwenye

hopsitali ya Misheni ya Mchukwi na chanzo cha ajali hiyo ni ni mwendo

wa kasi na ulevi uliopindukia wa dereva huyo ambaye alidaiwa kunywa

pombe alipofika Kibiti.



mwisho.

0 comments:

About This Blog

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP